Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:59

Odinga awasilisha kesi mahakamani


Waziri mkuu anayeondoka Raila Odinga akiwahutubia wafuasi wake Nairobi, Machi 16, 2013.
Waziri mkuu anayeondoka Raila Odinga akiwahutubia wafuasi wake Nairobi, Machi 16, 2013.

Waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi wa Kenya ulikuwa wa amani na matokeo yake yanaaminika.

Mgombea urais aliyeshindwa nchini Kenya Raila Odinga, amewasilisha kesi katika mahakama kuu jijini Nairobi Jumamosi kupinga matokeo ya kiti hicho yaliyotangazwa wiki jana.

Mapema Jumamosi polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kutawanya waandamanaji waliokusanyika nje ya mahakama kuu ya Kenya, kuunga mkono waziri mkuu anayeondoka Raila Odinga.

Muungano wa chama chake -CORD unasema una imani Bw. Odinga atashinda kesi hiyo. Bw. Odinga alikataa kukubali matokeo ya uchaguzi huo akidai kulikuwa na kasoro wakati wa kuhesabu kura.

Hapo awali Odinga alikuwa ameahidi kama wagombea urais wenzake ,kuwa ataheshimu matokeo ya kiti cha urais.

Tume huru ya uchaguzi Kenya, ilimtangaza Bw. Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa urais kwa kuzoa asili mia 50.07 ya kura na hivyo kuepuka uchaguzi wa marudio. Waangalizi wa kimataifa na wale wa ndani ya nchi walisema uchaguzi huo ulifanyika kwa njia ya amani na kwamba matokeo yake yanaaminika.
XS
SM
MD
LG