Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 08, 2024 Local time: 14:44

Obama awasili China katika mkutano wa G-20


Rais Barack Obama akiwasili Hangzhou mashariki mwa China, Sept. 3, 2016.
Rais Barack Obama akiwasili Hangzhou mashariki mwa China, Sept. 3, 2016.

Rais Barack Obama wa Marekani amewasili Hangzhou, China, Jumamosi mchana ambako ataungana na viongozi wengine wa nchi za kundi la G-20 kwa mkutano wao mkuu.

Obama anatazamiwa kukutana na rais Xi Jinping wa China kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

Baada ya mkutano wa G-20 Jumapili na Jumatatu, kiongozi huyo wa Marekani atakwenda Laos kuhudhuria mkutano wa ushirika wa mataifa ya kusini mashariki mwa Asia na Asia mashariki kuanzia Jumanne hadi Alhamisi.

Ban Ki-Moon, Xi Jinping na Obama mjini Hangzhou
Ban Ki-Moon, Xi Jinping na Obama mjini Hangzhou

Obama anakabiliwa na orodha ndefu ya maswala katika mkutano wa G-20 ambako viongozi kutoka nchi 20 zenye uchumi mkubwa zinatazamiwa kuwa na mjadala mgumu wa jinsi ya kuhamasisha uchumi wa dunia na kuboresha sera za mabadiliko ya hali ya hewa.

Obama alizungumza mjini Honolulu Alhamisi na kundi la viongozi wa nchi za Pacific, akiwaambia kuwa “Hakuna nchi, hata nchi kubwa kama Marekani, ambayo haitaathirika na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Katika mikutano yake mingine kando ya G-20 Rais Obama anatazamiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa Uturuki, Russia. Anatazamiwa pia kuwa na mazungumzo ya kwanza na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May Jumapili.

XS
SM
MD
LG