Viongozi hao wamekutana kwa mara ya kwanza moja kwa moja, ikionekana kuwa hatua kubwa kwenye juhudi za karibuni za maridhiano, baada ya kudorora kwa mahusiano hapo nyuma, ambapo wote wawili walirushiana maneno makali.
Kupitia ujumbe wa X iliyojulikana awali kama Twitter, maafisa wa Uturuki wametaja hatua hiyo kuwa muhimu, wakati mazungumzo yakiangazia suala la nishati. Ankara inakaribia Israel kama njia rashisi ya kusambaza gesi kutoka kwenye hifadhi zake nyingi, kuelekea Ulaya.
Waangalizi wanasema kwamba kuendelea kwa ushawishi wa kieneo wa Iran ni suala la kutia wasi wasi. Kuungwa mkono kwa Azerbaijan na wote Israel na Uturuki kunazua wasi wasi kuhusu Tehran, kwa kuwa inaunga mkono hasimu wa Azerbaijan, Armenia.
Ripoti zinasema kwamba Netanyahu na Edorgan wameahidiana kutembeleana hivi karibuni. Ripoti zinaongeza kusema kwamba Edorgan ambaye ni Muislamu, ameelezea azma yake ya kutembelea Jerusalem mwaka huu, na kusali kwenye msikiti wa al Aqsa ambao ni wa tatu kwa utakatifu kwenye dini ya Kiislamu.
Forum