Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 15:42

Ndugu wa Mohamed Bazoum wa Niger wanasema hawajasikia lolote kutoka kwake


Rais aliyepinduliwa wa Niger, Mohamed Bazoum. May 2, 2022.
Rais aliyepinduliwa wa Niger, Mohamed Bazoum. May 2, 2022.

Tangu alipopinduliwa na jeshi Julai 26, Bazoum amekuwa akizuiliwa katika makazi yake ya Rais yaliyopo katikati ya ikulu, pamoja na mkewe na mtoto wake.

Ndugu wa Rais aliyepinduliwa nchini Niger, Mohamed Bazoum siku ya Alhamisi walisema hawajasikia habari zozote kutoka kwake tangu Oktoba 18, wakilaani “ukamataji wa kudhalilisha na upekuzi” uliofanywa kwa baadhi yao.

Tangu alipopinduliwa na jeshi Julai 26, Bazoum amekuwa akizuiliwa katika makazi yake ya Rais yaliyopo katikati ya ikulu, pamoja na mkewe na mtoto wake. Licha ya wito unaoendelea kuhusu kuachiliwa kwake kutoka nchi na mashirika kadhaa, utawala mpya wa kijeshi wa Niger haukubaliani na hilo.

“Tangu Oktoba 18, hatujapata habari zozote za Rais Bazoum, mkewe Khadija Mabrouk na mtoto wao wa kiume Salem, ambao wametekwa nyara na walinzi wa rais”, familia yake ilisema katika taarifa.

Forum

XS
SM
MD
LG