Mtu mmoja nchini Namibia amefariki kutokana na homa ya kuvuja damu aina ya Crimean-Congo na kusababisha nchi hiyo kutangaza mlipuko wa ugonjwa huo, serikali imesema leo Jumatano. Ugonjwa huo pia unajulikana kama homa ya Congo, una kiwango cha juu cha vifo hadi asilimia 40 kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Kesi moja inachukuliwa kama mlipuko, mkurugenzi mtendaji wa wizara ya afya, Ben Nangombe aliliambia shirika la habari la AFP. Ugonjwa huu unasambaa kwa kung’atwa na kupe, na hivyo unaweza kuchukuliwa kama mlipuko wa ndani.
Mtu aliyeambukizwa alipelekwa kliniki katika mji wa mashariki wa Gobabis wiki iliyopita akiwa na dalili za ugonjwa huo, ambazo ni homa, maumivu ya misuli, kizunguzungu, kupata shida kutazama eneo lenye mwanga na kichefuchefu. Baadae aliwekwa karantini katika hospitali ya mji mkuu Windhoek mahala ambako alifariki.
Forum