Upatikanaji viungo

Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 21:38

Mlinzi wa amani wa Umoja wa Afrika ahukumiwa kifungo cha mwaka mmoja


Kenya Somalia
Kenya Somalia

Mlinzi wa amani wa Umoja wa Afrika amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na kushushwa cheo kwa kuuza vifaa vya kijeshi na petroli kwa magendo mjini Mogadishu.

Hukumu hii imeonekana wazi wakati kwa mara ya kwanza askari wa umoja wa Afrika AMISOM amehukumiwa mbele ya umma huko Somalia na mfano wa kipeke kwa askari kuadhibiwa kwa kuuza bunduki na silaha , ikiwa ni jambo la kawaida kwa wote AMISOM na maaskari wa jeshi la taifa la Somalia.

Mwanajeshi huyo wa Uganda Meja Pop Francis Origi alikuwa mmoja wa askari 18 wa Umoja wa Afrika walioshitakiwa jumanne kwenye mahakama ya kijeshi ya AMISOM kwa makosa kadhaa.Waandishi wa habari walialikwa kushuhudia kesi hizo.

Pamoja na hukumu hiyo Origi alishushwa cheo na kuwa Kapten.

XS
SM
MD
LG