Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:30

Mwanajeshi wa Israel auwawa Gaza.


wapalestina wakitoroka makazi yao kuhofia mashambulizi makali ya israel huko Rafah.
wapalestina wakitoroka makazi yao kuhofia mashambulizi makali ya israel huko Rafah.

Jeshi la Israel limesema mmoja wa wanajeshi wake amekamatwa na wanamgambo katika ukanda wa Gaza ambako sitisho la muda la mapigano lilivunjika masaa machache tu baada ya kuanza.

Maafisa wa kijeshi walinukuliwa na vyombo vya habari vya Israel wakisema kuwa tuhuma hizo za utekaji zilitokea kwenye mji kusini mwa Rafah baada ya makubaliano ya Amani ya kibinaadamu baina ya Israel na Hamas kuanza. Hakuna maelezo ya kina yaliyotolewa.

Muda mfupi baadae Isarel ilisema shambulizi lilitokea ambapo jeshi lake lililazimika kujibu mashambulizi hayo yaliyopelekea vifo vya wapalestina 27. Wanamgambo pia walianza tena kufyatua roketi kusini mwa Israel.

Ofisi ya waziri mkuu wa palestina Benjamin Netanyahu ilitoa taarifa ikilaumu wanamgambo wa Gaza kwa ukiukwaji wa makubaliano ya siku tatu ya kusitisha mapigano. Vyombo vya habari vya Israel vinaripoti kuwa makubaliano hayo yamevunjika na jeshi limeanza tena operesheni zake za ukandamizaji katika ukanda wa Gaza.

XS
SM
MD
LG