Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 12:09

Mwana wa waziri azuia ndege kutua


Ndege ya shirika la ndege la MEA ikitua LOndon
Ndege ya shirika la ndege la MEA ikitua LOndon

Shirika la ndege la MEA laeleza kwamba ndege yake iliyokuwa na abiria 71 ililazimika kurudi Beirut baada ya mtoto wa kiume wa waziri wa uchukuzi wa Iraq kuchelewa kuwasiili na hivyo kupiga simu Baghdad akitaka ndege hiyo izuiliwe kutua.

Ndege ya shirika la ndege la Mashariki ya Kati (MEA) iliyokuwa ikitoka Lebanon kuelekea Iraq ililazimika kurejea ikiwa katikati ya safari Alhamis, baada ya mtoto wa kiume wa waziri wa uchukuzi wa Iraq kuwasili uwanja wa ndege wakti ndege ilishaondoka na hapo alipiga simu Baghdad akiamrisha ndege hiyo isiruhusiwe kutua. .

Shirika hilo la ndege linasema ndege yake ililazimika kurudi Beirut baada ya kuwa angani kwa dakika 21.Ndege hiyo ya shirika la MEA ilichelewa kuondoka kwa dakika sita kwa sababu ya kumkosa abiria mmoja aliyetambulishwa na shirika hilo lenye makao yake Beirut, kama mwana wa kiume wa waziri wa uchukuzi wa Iraq Hadi al-Ameri.

Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 71 ilikataliwa kutua Baghdad na kurejea Beirut. Huko Baghdad, msemaji wa waziri mkuu Nouri al-Maliki alisema Bw. Maliki ameamrisha waliofanya maamuzi hayo wafutwe kazi.
XS
SM
MD
LG