Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Machi 26, 2025 Local time: 20:17

Mwalimu Fogel aliyekuwa anashikiliwa Russia akutana na Rais Trump ikulu


Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) akiwa White House na Mwalimu Marc Fogel.
Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) akiwa White House na Mwalimu Marc Fogel.

Rais wa Marekani Donald Trump amemkaribisha Mwalimu raia wa Marekani Marc Fogel katika white house siku ya Jumanne usiku.

Fogel alirejea nchini Marekani baada ya kuachiliwa huru kutoka Russia ambako amekuwa akizuiliwa tangu Agosti 2021, kwa tuhuma za kuingia Russia na bangi.

Fogel amesema kwamba anahisi ana bahati sana duniani.

Amemshukuru rais Trump na wanadiplomasia wa Marekani pamoja na mawakili kwa kusaidia kuweza kuwa uhuru.

Trump amesema anashukuru kwamba Russia ilimuachilia huru Fogel. Hata hivyo hajatoa taarifa zaidi kuhusu makubaliano yaliyopelekea Fogel kuachiliwa huru.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba Marekani ilikuwa imekubali kumuachilia huru raia wa Russia anayezuiliwa katika gereza la Marekani kama sehemu ya makubaliano hayo na kwamba aliyewachiliwa huru watatajwa atakapowasili R

Forum

XS
SM
MD
LG