Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 19:18

Rais Museveni awania tena uongozi nchini Uganda


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akikagua gwaride alipowasili bungeni kuhutubia kuhusu hali ya kitaifa katika mji mkuu Kampala, Juni 4, 2015.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni akikagua gwaride alipowasili bungeni kuhutubia kuhusu hali ya kitaifa katika mji mkuu Kampala, Juni 4, 2015.

Hivi karibuni katika makao makuu ya chama tawala cha NRM nchini Uganda, kulifurika wafuasi ambao walikuwa wakimsubiri kwa hamu kubwa Rais Yoweri Museveni. Aliwasili nyakati za mchana, bwana Museveni alilakiwa na umati mkubwa, na kuchukua fomu na kuthibitisha rasmi azma yake ya kupeperusha tena bendera ya urais kupitia NRM.

Bwana Museveni anawania awamu ya tano ya uongozi. Anasema ilikuwa ni uamuzi ambao yeye na wanachama waasisi wa NRM waliufanya pamoja. Bwana Museveni ni mgombea pekee ndani ya chama cha NRM.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:09 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hiyo ni kwasababu mpinzani wake, Amama Mbabazi, ameamua kuwania urais kama mgombea huru. Mbabazi amesema kwamba wakati bado ni mwanachama wa NRM, chama kinahitaji kujiangalia tena chenyewe, akikishutumu kuingilia kati ugombea wake.

Uamuzi wa bwana Museveni kuwania tena unakuja katikati ya matamshi ya karibuni ya Rais wa Marekani, Barack Obama kwa umoja wa Afrika kuwa hakuna mtu anatakiwa awe rais wa maisha. Makamu rais wa zamani wa Uganda, Gilbert Bukenya anakubaliana na hilo akisema bwana Museveni ni vyema afahamu hilo.

“ lazima ajue matokeo. Lazima afahamu kwamba hatuwezi kuruhusu udikteta. Lazima afahamu kwamba watu wamechoshwa na kiongozi wa muda mrefu ambaye alikuwa akiwaeleza wengine kwamba wamekuwepo kwa muda mrefu wakati ambapo hawakukaa kwa zaidi ya miaka 10,” anaelezea Bukenya.

Hata hivyo, pongezi nyingi zinakwenda kwa uongozi wa bwana Museveni kwa kuleta uthabiti na ukuaji wa uchumi. Mfuasi wa muda mrefu na msaidizi wa naibu rais, Duncan Abigaba anaelezea kwanini.

“ Watu wanampongeza kwa kuleta Amani na usalama kwasababu hakuna hata wakati mmoja katika nchi hii, katika historia ya nchi ambapo kulikuwa na amani. Kwahiyo watu hivi sasa hawana wasi wasi, wanasema ndiyo hatuna fedha mifukoni, lakini Museveni ametuletea amani, na ninaweza kuitumia amani ninavyotaka. Kwahiyo Museveni ni vyema abakie,” anasema Abigaba

Wakati kinyang’anyiro cha kuwania urais cha Museveni kiko wazi, Mbabazi bado kuna giza. Kuna uvumi kwamba atajiunga hapo baadaye na Democratic Alliance ushirika wa vyama vya siasa vya upinzani. Ushirika nao unasema wako wazi kumpokea Mbabazi, ingawaje mitaani bado ana kazi kubwa ya kufanya kuweza kuibeba bendera ya Democratic Aliance.

XS
SM
MD
LG