Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemfukuza kazi Makamu wa Rais Joice Mujuru na mawaziri saba wa serikali walioaminika kuwa washirika wake.
Katika mahojiano na Sauti ya Amerika, Mujuru amesema amekubaliana na shauri la Rais Mugabe la kuachia madaraka.
Vilevile Mujuru amekanusha shutuma za kwamba alikuwa anapanga njama za kumuondoa madarakani Rais Mugabe na kusema ataendelea kuwa mwanachama muaminifu wa chama tawala cha ZANU-PF.
Kuna wakati alionekana kama mtu atakayemrithi Mugabe mwenye umri wa miaka 90, vilevile Mujuru amepoteza wadhifa wake wa umakamu mwenyekiti wa ZANU-PF katika mkutano uliopita.
Hatua hiyo imefuatia shutuma kutoka kwa mke wa Rais, Grace Mugabe kwamba hakuwa mtu sahihi wa kuongoza nchi. Bibi Mugabe, amewekwa kama mkuu mpya wa chama katika kitengo cha wanawake.