Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 07:18

Muathiriwa wa ubakaji afariki


Indians gather next to a makeshift memorial to mourn the death of a 23-year-old gang rape victim, in Bangalore, India , Saturday, Dec. 29, 2012.
Indians gather next to a makeshift memorial to mourn the death of a 23-year-old gang rape victim, in Bangalore, India , Saturday, Dec. 29, 2012.
Mwanafunzi wa kike nchini India aliyebakwa na genge la watu akiwa kwenye basi mjini New Delhi amefariki dunia katika hospitali moja ya Singapore. Taarifa kutoka hospitali hiyo ya Mount Elizabeth ilisema mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 23 aliaga dunia mapema Jumamosi. Waziri mkuu wa India Manmohan Singh alisema amehuzunishwa sana na kifo cha msichana huyo. Alisema jazba zinazotokana na kubakwa kwake na sasa kifo chake zinaeleweka. Maiti ya mwanamke huyo imrejeshwa India Jumamosi. Mji wa New Delhi umekubwa na maandamano na ghasia tangu shambulizi hilo la kikatili. Maafisa mjini humo wanasema wanajiandaa kukabiliana na maandamano na ghasia zaidi kufutia kifo chake. Mwanamke huyo alikuwa akisafiri katika basi Desemba 16 na rafiki yake wa kiume wakati waliposhambuliwa na wanaume sita waliokuwa ndani ya basi hilo. Walipigwa kwa kutumia vyuma na kisha mwanamke huyo kubakwa na wanaume hao. Yaripotiwa pia walimuumiza vibaya kwenye sehemu zake za siri kwa kutumia chuma na kwamba vipigo alivyopata vilisababisha majeraha kwenye ubongo wake. Hatimaye mwanamke huyo na rafikiye wa kiume walitupwa nje ya basi likiwa bado linakwenda.
XS
SM
MD
LG