Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 22:14

Mtwara watofautiana na serikali kuhusu bomba la gesi


Mitambo ya kuchimba mafuta
Mvutano mkubwa umezuka nchini Tanzania baina ya serikali na wananchi wanaotoka mkoa wa Mtwara ambao wanapinga hatua ya serikali kuweka bomba litakolotumika kusafirisha gesi kutoka mkoani humo hadi mkoani Dar es Salaam.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:55 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wakati serikali ikiendelea kusisitiza nia ya kuendelea na hatua hiyo mamia ya wananchi wa mkoa wa Mtwara wakiungwa mkono na wabunge wao wanaitaka serikali kusitisha zoezi hilo na badala yale uendeshwaji wa gesi hiyo ufanyike ndani ya mkoa wa Mtwara eneo ambalo limegunduliwa kuwa na gesi nyingi nchini humo.

Tayari Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospita Mhongo wamezungumzia sakata hilo na kuwataka wananchi hao kuyaweka kando madai yao kwa maelezo kuwa rasilimali zinazoendelea kugundulika ndani ya nchi zitatumika kwa manufaa ya wananchi wote.

Mvutano kuhusu wapi iendelezwe gesi hiyo umezidi kuchukua sura mpya baada ya hivi sasa kujitokeza viongozi wa kidini na kutangaza kuwa wanaunga mkono madai yaliyotolewa na wananchi wa mkoa wa Mtwara ambao wanasisitiza kuwa wananyang’anywa rasilimali zao.

Kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amezitolea wito pande zote kuwa na majadiliano ya pamoja na hatimaye kutoa suluhisho litakolosaidia uendelezwaji wa rasilimali hiyo.

Wakati huo huo makundi ya wanaharakati hivi karibuni yalikutana na kujadiliana kwa kina sera mpya iliyotolewa na serikali kuhusu sekta ya gesi. Pamoja na mambo mengine makundi hayo ya wanaharakati yalikosoa na kuipinga sera hiyo wakidai kuwa imejaa mapungufu.

Wananchi wa eneo la Mtwara pia wameokosoa sera hiyo kwa madai kuwa hawakushirikishwa wakati wa kuandaliwa kwake.

Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala cha CCM, wameunga mkono madai yanayotolewa na wananchi hao na wengine wakisisitiza kuwa wako tayari kuchukuliwa hatua zozote na chama lakini wataendelea kutetea hoja za wananchi wao.
XS
SM
MD
LG