Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 02:48

MRC waendelea kusakwa na serikali ya Kenya


Wanachama wa kundi la MRC wakiandamana Mombasa siku za nyuma.
Wanachama wa kundi la MRC wakiandamana Mombasa siku za nyuma.
Mamlaka nchini Kenya hawajasitisha msako dhidi ya viongozi na wafuasi wa vuguvugu la Mombasa Republican Council( MRC) kwa madai ya uchochezi na kudai kuwa eneo la Pwani sio sehemu ya Kenya. Mtu aliyesakwa na polisi kwa miezi mitatu amekamatwa na kushtakiwa, huku viongozi wa MRC wakidai kuna njama ya kuhakikisha serikali inaendelea kuwakamata.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:47 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Mombasa Josephat Kioko anaripoti kuwa zaidi ya wanachama 50 wa Mombasa Republican Council walitiwa mbaroni mwaka uliopita wa 2012, wakiwemo viongozi kadhaa. Kamata ,kamata hiyo ilichacha katika sehemu zilizosheheni vurugu na mauaji ya watu kadhaa, na vitisho kwa raia.

Mtu aliyekuwa akisakwa na polisi kwa miezi mitatu sasa - Salim Ali Konga amefikishwa katika mahakama moja hapa Mombasa, kujibu mashtaka ya uchochezi, akiitwa kiongozi wa MRC. Salim alitakiwa kujisalimisha pamoja na wanachama wengine wa MRC wakiongozwa na mwenyekiti wao Omar Mwamnuazi mwishoni mwa mwaka uliopita.

Lakini baada ya kufikishwa kortini Jumatatu asubuhi, amesema kuwa polisi wamekosea, kwa kufananisha jina lake na mtu wanayemsaka. Mahakama itaamua kesho baada ya kukagua stakabadhi za polisi wanaongoza mashtaka.

Miongoni mwa watu waliofika mahakamani Mombasa kufuatilia kesi hiyo, ni pamoja na Msemaji wa Mombasa Republican Council ,Rashid Mraja, ambaye pia ana kesi ya kama hiyo ya uchochezi, ambapo miezi miwili iliyopita aliwekwa gerezaji kwa zaidi ya siku 10.

Katika mazungumzo na wanahabari nje ya mahakama, Mraja amekana madai kwamba wanachama wao wanapanga kuzuia uchaguzi mkuu,kufanyika Pwani ya Kenya. Msemaji huyo wa wa MRC amedai hii ni njama tu inayoenezwa kuashiria madai hayo, na kwamba inanuia kusukuma serikali kuwasaka na kuwakamata tena wanachama wa kundi hilo.

Lakini uhalali wa kundi la MRC unaonekana kugawanya viongozi, wanasiasa kadhaa wamenukuliwa wakishinikiza mazungumzo na serikali, lakini ndani ya serikali yenyewe hilo likipingwa.

Mkuu wa mkoa wa Pwani Samuel Kilele anaongoza kamati ya Usalama mkoani humo na amesema ikiwa serikali ilifanikiwa kutokomeza al-Shabab Somalia, seuze wanachama wa MRC ndani ya Kenya? Mwezi mmoja uliopita mahakama kuu ilitupitia mbali kesi ya vuguvugu la MRC ya kutaka serikali iidhinishe kura ya maoni kuhusu uhalali wao, na tayari wamekata rufaa kupinga uamuzi huo.
XS
SM
MD
LG