Moto katika jengo la ghorofa lililopo katika moja ya vitongoji vya zamani huko Dubai umesababisha vifo vya watu 16. Watu tisa walijeruhiwa katika moto huo maafisa walisema Jumapili.
Watu wengi wanajulikana kuishi katika nyumba za jengo hilo na maeneo jirani. Ni utaratibu wa kawaida miongoni mwa vibarua wa jiji kugawanya vyumba vyao katika ukubwa wa wastani ili kusaidiana kimaisha ambapo mara nyingi hutumia mapazia ya bafuni na ubao wenye fito nyembamba mojawapo ya vitu vinavyoweza kuwa hatari kubwa ya chanzo cha moto.