Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 07:17

Morsi akutana na Catherine Ashton


Rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi na mkuu wa EU Catherine Ashton
Rais wa zamani wa Misri Mohammed Morsi na mkuu wa EU Catherine Ashton
Wafuasi wa rais aliyetimuliwa madarakani nchini Misri Mohammed Morsi wameitisha maandamano zaidi Jumanne huku mwanadiplomasia wa ngazi ya juu katika Jumuiya ya Ulaya akisema kiongozi huyo wa zamani anaishi vizuri japo amezuiliwa.

Mkuu wa Jumuiya hiyo ya Ulaya Catherine Ashton alisema amezungumza na bw. Morsi kwa njia ya wazi kuhusu mzozo wa kisiasa uliogubika Misri. Bi Ashton alisema mojawapo ya masharti aliyowekea utawala wa muda katika ziara yake ya Misri, ni kuweza kuzungumza na bw. Morsi.

Maafisa nchini humo walimpa nafasi ya kuzungumza na rais huyo wa zamani kwa muda wa saa mbili lakini Ashton hakuweza kubaini ni wapi Mosri anazuiliwa.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwanadiplomasia wa kimataifa kukutana na kiongozi huyo aliyetimuliwa tangu majeshi ya Misri yalipomkamata na kumweka kizuizini yapata mwezi mmoja uliopita.
XS
SM
MD
LG