Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 03:30

MONUSCO yawalaumu FDLR kukwamisha utaratibu wa kutua silaha chini


Wanajeshi wa MONUSCO kwenye kituo kimoja cha ukaguzi nchini DRC
Wanajeshi wa MONUSCO kwenye kituo kimoja cha ukaguzi nchini DRC

Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Kongo-MONUSCO imelaumu wapiganaji wa kundi la FDLR kwa kukwamisha utaratibu wao wa kuweka chini silaha. Naibu kiongozi wa tume ya MONUSCO,alisema wapiganji wa FDLR wameonyesha nia mbaya katika kutafuta amani.

Naibu kiongozi wa MONUSCO, Jenerali Abdallah Waffi alisema taratibu za kutua chini silaha kwa wapiganaji wa Rwanda wa FDLR imekwama kutokana na sababu zao wenyewe. Bwana Waffi alisema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari. Aliongeza kwamba wapiganaji hao wamekaidi kupelekwa nje ya majimbo ya Kivu. “Washiriki kwenye mkutano wa kutahimini taratibu ya kujisalimisha kwa wapiganaji hao,wamekubaliana kwamba taratibu hiyo imekwama.Na wanaokwamisha utaratibu huu ni wapiganaji wenyewe wa FDLR ambao wamegoma kupelekwa nje ya majimbo ya Kivu. Kiongozi wao ali-iandikia barua jumuiya ya SADC kwamba hawataondoka Kivu kwa vyovyote vile hadi hapo masharti yao yatakapokamilika”.

Jenerali Abdalah waffi alisema kwamba msimamo huo wa wapiganaji wa FDLR unaonyesha nia mbaya ya kutotoa ushirikiano katika juhudi za Amani. “ Serikali ya Kongo kwa ushirikiano na MONUSCO walichukuwa hatua za kuwasafirisha wapiganaji ambao walijisalimisha wenyewe hadi Kisangani kabla ya kupewa mahala pengine pa kuishi. Lakini wamekataa japokuwa wamerudishwa na kuhudumiwa na MONUSCO lakini hawatuamini”.

Marais wa nchi za maziwa makuu waliwapa ilani ya miezi sita wapiganaji hao wa FDLR iliwajisalimishe kwa hiyari yao wenyewe la sivyo watalazimishwa kwa nguvu.

Katika kutafuta suhulisho juu ya suala hilo mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya maziwa makuu Russ Feingold yuko ziarani huko mashariki mwa Kongo. Akiwa mjini Goma bwana Russ alisema kwamba nchi yake itaendelea kushirikiana pamoja na serikali ya Kongo katika kuyamaliza makundi yote ya wapiganaji likiwemo lile la FDLR. Mjumbe huyo wa Marekani alisema kwamba suala la FDLR limepitwa na wakati na ni lazima sasa kufungua ukarasa mpya wa ujenzi wa Kivu.

Ziara hiyo itampeleka pia mjini Bukavu katika jimbo la Kivu kusini. Alianza safari yake kutokea Kigali nchini Rwanda. Wiki ijayo anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kundi la marafiki wan chi za maziwa makuu utakaofanyika mjini London, Uingereza.

XS
SM
MD
LG