Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 15:58

Mlipuko wa kipindupindu waripotiwa Afika Kusini


Mtoto akitibiwa kipindupindu kwenye hospitali. Picha ya maktaba
Mtoto akitibiwa kipindupindu kwenye hospitali. Picha ya maktaba

Maafisa wa afya wa Afrika Kusini wameripoti mlipuko mbaya wa kipindupindu kwenye jimbo la Gauteng.

Ripoti zinaongeza kusema kwamba karibu watu 50 wamekufa, vifo vingi vikitokea kwenye eneo la Hammanskraal, ingawa visa vya maambukizi vimeripotiwa kwenye sehemu nyingine pia.

Maafisa wa afya wameomba wakazi kuwa waangalifu kuhusu wanachokula pamoja na kuzingatia usafi kwa kuwa kipindupindu kinaenezwa kupitia uchafu kwenye chakula au maji. Dalili zake ni pamoja na kuharisha, kutapika na ukosefu wa maji mwilini.

Forum

XS
SM
MD
LG