Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:01

Mkataba wa amani DRC


Rais wa DRC Joseph Kabila, (kulia),Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda mjini Kampala.
Rais wa DRC Joseph Kabila, (kulia),Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda mjini Kampala.
Mjumbe wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anasema raia wa Congo wanafuraha juu ya uwezekano wa kupatikana amani kufuatia ripoti kuwa serikali ya Kinshasa itatia saini makubaliano na waasi wa M23 hii leo Jumatatu.

Bebe M’poko balozi wa DRC huko Afrika Kusini anasema serikali ya DRC inapanga kudhibiti zaidi usalama kwenye mipaka yake ili kuwalinda raia wasio na silaha kutokana na mashambulizi ya makundi mengine yenye silaha. Alisema mzozo wa taifa hilo unachangiwa pia na wale ambao wanataka kuizuia DRC kunufaika na raslimali zake kubwa.

Bw M’poko anasema vita hivyo vinaendelea kwa sababu kuna watu ambao wanataka kupora raslimali za Congo na kuiweka Congo katika hali isiyo thabiti.

Anasema raslimali hizo zingewanufaisha watu wa Congo, bara la Afrika na hata ulimwengu mzima, kwa sababu Congo ni eneo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini, mafuta, utalii na kadhalika.

Anasema jeshi la congo litaweza kulinda mipaka ya nchi hiyo ambayo imekuwa wazi na hivyo kuwezesha makundi yenye silaha kuingia kutoka nchi jirani.

Wote DRC na kundi la waasi wa M23 wanatarajiwa kutia saini makubaliano ya amani hii leo, katika mji mkuu wa Kampala, Uganda. Hatua hiyo inafuatia miezi ya majadaliano baina ya pande hizo mbili na tangazo la kundi la M23 kuwa linaweka chini silaha zao, baada ya vikosi vya jeshi la DRC kuwan’goa kutoka ngome zao zilosalia wiki jana.
XS
SM
MD
LG