Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:21

Mjadala wa rasimu ya katiba Tanzania umekwama: Profesa Lipumba


Ndani ya Bunge la taifa la Tanzania
Kikao cha Bunge la Katiba kimeahirishwa hadi mwezi wa Ogusti, ambapo wajumbe Tatajaribu kuanza tena mjadala wa kuidhinisha rasimu ya katiba iliyowasilishwa na tume ya Mabadiliko ya katiba.

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Profesa Ibrahim Lipumba, kiongozi wa chama cha upinzani cha CUF, na mjumbe katika Bunge Maalum la Katiba anasema mjadala wa rasimu ya katiba umekwama "kwani tangu tumeingia, tumeanza majadiliano kwa karibu siku 70 hatujaweza kupitisha hata kifungu kimoja cha katika"
please wait

No media source currently available

0:00 0:13:16 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Anasema, "kwa kweli mapendekezo yanayojitokeza yanabadilisha kabisa kiini cha mapendekezo ya katiba yaliyopendekezwa na tume ya mabadiliko ya katiba".

Profesa Lipumba anamlaumu Rais Jakaya Kikwete kuvuguga kabisa utaratibu wa majadiliano kutokana na hotuba yake ya kufungua kikao cha Bunge Maalum ya Katiba akikejeli kazi iliyofanywa na tume ya Warioba aliyeichagua mwenyewe.

Wajumbe wa upinzani katika bunge hilo la katiba, walounga mungano wa UKAWA wameruhusiwa kuanda mikutano ya hadahra kufafanua kilichoendelea katika bunge na kueleza wananchi ka nini wanapinga maoni yasiyoambatana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
XS
SM
MD
LG