Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:42

Mimi nasema muwapige tu: Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.


Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.
Kauli ya waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda bungeni Dodoma katika mabishano kuhusu matumizi ya nguvu yanayofanywa na jeshi la Polisi nchini humo ilitolewa bungeni alhamisi wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kutoka kwa mbunge wa Kilwa Kaskazini Murtaza Mangungu .

Waziri mkuu huyo alijibu “Ukifanya fujo umeambiwa usifanye hiki ukaamua wewe kukaidi utapigwa tu maana hakuna namna nyingine maana wote lazima tukubaliane nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria sasa kama wewe umekaidi hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi watakupiga tu na mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine maana tumechoka sasa”.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:49 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Nao wanaharakati wa haki za binadamu wamezungumza juu ya kauli hiyo Sauti ya Amerika ilizungumza na mtetezi wa haki za binadamu Prugensi Massawe wa kituo cha sheria na haki za binadamu ambaye amehoji kauli hiyo ya waziri mkuu. Akielezea kila kitu kimeainishwa kwenye sheria kwasababu Tanzania ni nchi yenye utawala wa sheria.
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:25 0:00
Kiungo cha moja kwa moja
XS
SM
MD
LG