Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:24

Mgonjwa anayeshukiwa kuugua Ebola alazwa New York


Hospitali ya Mount Sinai, New York
Hospitali ya Mount Sinai, New York

Maafisa katika hospitali ya Mount Sinai wanasema mtu mmoja mwenye homa kali na maumivu ya tumbo aliwasili hospitalini Jumatatu asubuhi na kutengwa na wagonjwa wengine mara moja.

Hospitali moja ya New York inampima mtu mmoja ambaye ana uwezekano wa kuwa na ugonjwa wa Ebola wakati idadi ya waliofariki dunia kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo huko Afrika Magharibi ikiongezeka na kufikia 900.

Maafisa katika hospitali ya Mount Sinai wanasema mtu mmoja mwenye homa kali na maumivu ya tumbo aliwasili hospitalini Jumatatu asubuhi na kutengwa na wagonjwa wengine mara moja.

Anasema mgonjwa huyo hivi karibuni alisafiri kwenda nchi moja ya Afrika magharibi ambako Ebola imeripotiwa na anafanyiwa vipimo kubaini ikiwa anaugua ugonjwa huo. Hakuna taarifa nyingine juu ya mtu huyo zilizotolewa.

Wakati huo huo, maafisa wa Nigeria wameripoti jana kuwa kesi ya pili ya Ebola imethibitishwa. Daktari aliyemtibu mgonjwa wa kwanza aliyefariki Julai 25 aliambukizwa ugonjwa huo hatari.

XS
SM
MD
LG