Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 14:31

Polisi wanane wa Tunisia wahukumiwa vifungo vya jela kwa kuhatarisha usalama wa umma


 Polisi waKIwasukuma nyuma wafuasi wa chama cha upinzani nchini Tunisia cha Ennahda wanaoandamana kuunga mkono viongozi wa chama chao anaokabiliwa na kuhojiwa na polisi wa kupambana na ugaidi mjini Tunis, Tunisia Septemba 19, 2022. REUTERS/Jihed Abidellaoui
Polisi waKIwasukuma nyuma wafuasi wa chama cha upinzani nchini Tunisia cha Ennahda wanaoandamana kuunga mkono viongozi wa chama chao anaokabiliwa na kuhojiwa na polisi wa kupambana na ugaidi mjini Tunis, Tunisia Septemba 19, 2022. REUTERS/Jihed Abidellaoui

Jaji mmoja wa Tunisia amewafunga jela wanachama wanane wa chama kimoja cha wafanyakazi cha polisi kwa kuhatarisha usalama wa umma na utovu wa nidhamu baada ya mapambano na maafisa wa polisi waliojaribu kuvunja maandamano yao afisa wa chama hicho alisema Ijumaa.

Mivutano imekuwa ikiongezeka kati ya vyama vya wafanyakazi vya polisi na Wizara ya Mambo ya Ndani. Muungano wa vyama vya wafanyakazi vya polisi unawashutumu maafisa wa serikali kwa kujaribu kukandamiza shughuli za vyama vyao, ambavyo vinasema ni mafanikio muhimu yaliyopatikana tangu mapinduzi ya 2011.

Hii inatokea wakati Rais Kais Saied anakosolewa vikali kwamba anazidi kuimarisha mamlaka yake baada ya kunyakua madaraka kamili mwaka jana, alipolivunja bunge, kutaja tume mpya ya uchaguzi na kuchukua nafasi ya Baraza Kuu la Mahakama katika hatua ambazo wapinzani wake wanasema ni mapinduzi.

Saied anakanusha shutuma hizo, anasema anatafuta tu kuunda jamhuri mpya ambayo itamaliza miaka mingi ya machafuko, uvunjaji wa sheria, ukosefu wa haki na ufisadi uliokithiri.

XS
SM
MD
LG