Mgomo huo ulioanza siku ya Ijumaa, umesababisha shida katika safari za ndege kote kwenye kanda hiyo na kuwaacha mamia ya abiria wakikwama katika viwanja vya ndege siku ya Jumamosi.
Muungano wa Vyama vya Waongoza ndege (USYCAA), ambao uliitisha mgomo huo, ulisema katika taarifa yake kwamba umeamua kusitisha mgomo usio idhinishwa kwa siku 10 ili kuruhusu mazungumzo yaendele.
Huduma za kuongoza ndege zitatolewa katika safari zote za anga na viwanja vya ndege vinavyosimamiwa na ASECNA kuanzia leo Jumamosi, Septemba 24, 2022 ilisema taarifa hiyo.
Waongoza ndege hao wanafanya kazi chini ya Wakala wa Usalama wa Anga barani Afrika na Madagascar (ASECNA).