Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 22:36
VOA Direct Packages

Mazungumzo ya nyuklia ya Iran na UN kuchua muda zaidi ya ilivyotarajiwa


Mkuu wa idara ya kimataifa ya nishati ya nyuklia IAEA Rafael Grossi kwenye picha ya awali mjini Vienna, Austria, March 6, 2023.
Mkuu wa idara ya kimataifa ya nishati ya nyuklia IAEA Rafael Grossi kwenye picha ya awali mjini Vienna, Austria, March 6, 2023.

Mku wa idara ya kimataifa ya nishati ya Atomic, IAEA, Rafael Grossi amesema Jumatatu kwamba makubaliano ya ushirikiano wa Iran na Umoja wa Mataifa wakati wa ziara yake mji Tehran mwishoni mwa wiki, yatategemea mashauriano zaidi katika siku zijazo.

Taarifa hiyo inaoekana kuenda kinyume na baadhi ya matamshi aliyotoa muda mfupi baada ya kukamilisha ziara yake. Ikiwa imebaki siku mbili kabla ya mkutano wa robo mwaka wa bodi ya IAEA yenye mataifa 35 wanachama, idara hiyo na Iran walikuwa wamesema kwamba wamepiga hatua kadhaa ikiwemo uchunguzi uliokwama wa chembechembe za uranium zilizopatikana kwenye viwanda vitatu nyuklia vya Iran.

Jumamosi Grossi alikuwa amesema kwamba walikubaliana kurudisha vifaa vya uangalizi kama vile kamera kwenye viwanda vya nuclear vya Iran vilivyoko chini ya mkataba wa Iran wa 2015, na mataifa yenye nguvu ulimwenguni, na ambao ulisitishwa mwaka jana kufuatia Marekani kujiondoa 2018.

XS
SM
MD
LG