Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 13, 2025 Local time: 23:21

Mazungumzo ya Bashir na Kiir yazaa matunda


Rais wa Sudan Omar al-Bashir (R) na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) kwenye mazungumzo ya masuala muhimu ya nchi zao
Rais wa Sudan Omar al-Bashir (R) na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (L) kwenye mazungumzo ya masuala muhimu ya nchi zao

Majeshi kutoka pande zote yanatakiwa kurudi nyuma kilomita 10 kutoka eneo la mpaka linalozozaniwa.

Marais wa Sudan na Sudan Kusini wanatia saini Alhamis mkataba unaolenga kuzuia vita vingine kutokea japokuwa baadhi ya masuala makuu bado hayajatatuliwa.

Maafisa katika serikali hizo wanasema mkataba huo uliopatikana baada ya mazungumzo katika mji mkuu wa Ethiopia unataka majeshi kutoka pande zote kurudi nyuma kilomita 10 kutoka eneo la mpaka linalozozaniwa.

Gazeti moja nchini Sudan la Sudan Vision linamkariri afisa mmoja ambaye ni balozi wa Sudan, Abdul Rahman Sir Al Khatim, akisema pande hizo pia zimeafikiana mikataba juu ya masuala ya usalama na mafuta.

Nchi hizo mbili bado zinatofautiana juu ya nani anayedhibiti eneo la Abyei lenye utajiri wa mafuta na maeneo mengine ya mpaka.

Mwandishi wa habari mmoja wa Sauti ya Amerika-VOA mjini Addis Ababa anasema sherehe za utiaji saini zilichelewa Alhamis lakini Rais Omar al-Bashr wa Sudan na Salva Kiir wa Sudan Kusini wanatarajiwa kutia saini makubaliano hayo kama ilivyopangwa.

Kaskazini na Kusini walipigana miaka 21 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo hatimaye vilipelekea kupatikana uhuru wa Kusini mwezi Julai mwaka 2011.
XS
SM
MD
LG