Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 19:19

Mazungumzo ya amani juu ya Ethiopia yameongezewa muda


Waandamanaji wakionyesha mabango kuhusu mazungumzo ya kutafuta amani Ethiopia yanayofanyika nchini Afrika kusini
Waandamanaji wakionyesha mabango kuhusu mazungumzo ya kutafuta amani Ethiopia yanayofanyika nchini Afrika kusini

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na Umoja wa Afrika yanataka kusitishwa kwa uhasama katika vita ambavyo Marekani inadai vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, makadirio yaliyotolewa na baadhi ya wasomi na wafanyakazi wa afya

Mazungumzo ya amani kati ya pande zinazozozana kuhusu mzozo wa Tigray nchini Ethiopia yameongezewa muda hadi leo Jumatatu.

Afisa anayefahamu mipango ya mazungumzo hayo anathibitisha kuwa majadiliano yanaendelea nchini Afrika Kusini kati ya serikali ya shirikisho ya Ethiopia na wawakilishi kutoka mkoa wa kaskazini wa Tigray.

Mazungumzo hayo yanayoongozwa na Umoja wa Afrika yanataka kusitishwa kwa uhasama katika vita ambavyo Marekani inadai vimesababisha vifo vya maelfu ya watu, makadirio yaliyotolewa na baadhi ya wasomi na wafanyakazi wa afya.

Mazungumzo ya kwanza rasmi ya amani yalianza wiki iliyopita, na serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imesema yangemalizika Jumapili. Wawakilishi wa pande zinazozozana hawajajibu maswali.

Nchi jirani ya Eritrea, ambayo vikosi vyake vinapigana pamoja na vile vya Ethiopia, sio sehemu ya mazungumzo hayo, na haijulikani ikiwa nchi hiyo kandamizi itaheshimu makubaliano yoyote yaliyofikiwa. Walioshuhudia wameliambia shirika la habari la AP kwamba Eritrea walikuwa wakiwaua raia hata baada ya mazungumzo hayo kuanza.

XS
SM
MD
LG