Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:27

Mazungumzo mapya ya amani kuanza tena Afghanistan

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilikutana katika mkutano wake wa kawaida kuhusu hali hiyo nchini Afghanistan masaa kadhaa baada ya washambuliaji wa Taliban kulipua bomu kubwa ndani ya gari nje ya mkutano wa bunge uliokuwa unajadili kumthibitisha waziri mpya wa ulinzi.

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa kwa ajili ya Afghanistan amekaribisha nia mpya ya mazungumzo ya amani baina ya serikali na kundi la Taliban lakini amesema hayawezi kufanyika bila kuhusishwa moja kwa moja baina ya pande husika.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilikutana katika mkutano wake wa kawaida kuhusu hali hiyo nchini Afghanistan masaa kadhaa baada ya washambuliaji wa Taliban kulipua bomu kubwa ndani ya gari nje ya mkutano wa bunge uliokuwa unajadili kumthibitisha waziri mpya wa ulinzi.

Maafisa wa usalama walisema washambuliaji wote saba waliuwawa. Hakuna mbunge aliyejeruhiwa, lakini maafisa wanasema takriban watu wengine 30 walijeruhiwa. Walikuwa miongoni wa raia 4,216 wa Afghanistan ambao umoja wa mataifa umesema waliuwawa au kujeruhiwa mwaka huu.

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa nchini Afghanistan , Nicholas Haysom aliliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba vikosi vya usalama nchini humo vilivyochukua udhibiti kutoka kwa vikosi vya kimataifa mwanzoni mwa mwaka huu bado vinaendelea kujaribiwa.

Amesema wapiganaji wa kigeni kutoka majirani wa kaskazini mwa Afghanistan na kwingineko wanatoa changamoto . Bado kuna hofu kuhusu ISIL wanaojulikana nchini Afghanistan kama Daesh wanajitahidi kuimarisha ngome yao. Amesema ushirikiano thabiti wa eneo ni muhimu kutatua vitisho hivyo.

XS
SM
MD
LG