Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 06:27

Mashambulizi yafanywa Nigeria


Mkusanyiko wa watu baada ya mlipuko wa bomu huko Kano, Nigeria, hii ilikuwa Novemba 28, 2014.

Washukiwa wakislam wenye msimamo mkali wameshambulia miji mikuu miwili ya kaskazini mashariki mwa Nigeria, Jumatatu wakilenga soko lenye mkusanyiko mkubwa wa watu na eneo la polisi.

Mashuhuda katika miji ya majimbo ya Maiduguri na Borno wamasema milipuko ilitokea katika soko lenye mkusanyiko mkubwa wa watu ambapo wanawake wawili walijitoa muhanga na kuua darzeni ya watu wiki moja iliyopita.

Haijafahamika ni watu wangapi wamekufa ama wamejeruhiwa katika mlipuko wa leo. Mashuhuda wanasema wamewaona watu wakitokwa na damu na kukosa viungo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP karibu watu kumi wamekufa katika mlipuko wa leo. Inasemekana waliojitoa muhanga walikuwa wanawake wawili.

Mapema Jumatatu wakazi wa Damaturu mji mkuu wa jimbo la Yobe wamesema wanaosadikiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram walishambulia eneo la polisi katika mji huo.

XS
SM
MD
LG