Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 13:45

Waumini 19 wauwawa Nigeria


Mtu akikagua mabaki kutokana na mlipuko wa bomu mjini Jalingo, Nigeria, April 30, 2012.
Mtu akikagua mabaki kutokana na mlipuko wa bomu mjini Jalingo, Nigeria, April 30, 2012.
Watu wenye silaha wamewafyatulia risasi waumini waliokuwa kwenye ibada kanisani jumanne huko kusini mwa Nigeria na kuwauwa watu wasiopungua 19 na kuwajeruhi kadhaa wengine.

Maafisa wa serikali ya Nigeria wanasema idadi ya watu wasiojulikana waliokuwa na silaha walilishambulia kanisa la Deeper Life huko Okene katika jimbo la Kogi. Maafisa wa usalama wanawatafuta washambuliaji lakini hawajafanikiwa kumkamata mtu yeyote. Hakuna mtu yeyote anayedai kuhusika na shambulizi hilo.

Kundi la ki-islam lenye msimamo mkali la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulizi kwenye makanisa kadhaa huko kaskazini na kati kati ya Nigeria katika kipindi cha mwaka uliopita lakini Okene ipo kusini zaidi ya eneo linalolengwa na kundi hilo.
XS
SM
MD
LG