Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 09:54

Marekani yaripoti mgonjwa wa kwanza wa Ebola


Hospitali ya Presbyterian, Dallas,Texas alikolazwa Thomas Eric Duncan

Idara ya afya imewaagiza watu wanne wa familia ya mgonjwa huyo anayetambuliwa kama Thomas Eric Duncan kutotoka nyumbani kwa siku 21 ili hali yao ya afya iweze kufuatiliwa kwa karibu.

Maafisa wa afya kutoka jimbo la Texas, Marekani wanachunguza watu 80 ambao walikuwa na mawasiliano ya karibu na mwanamume mmoja wa Liberia ambaye ameugua ugonjwa wa Ebola, huyu akiwa mgonjwa wa kwanza Marekani kugunduliwa na kirusi cha Ebola.

Msemaji wa idara ya afya katika kaunti ya Dallas Erikka Neroes, anasema hakuna anayeonyesha dalili za ugonjwa huo miongoni mwa watu hao 80 . Lakini idara hiyo imewaagiza watu wanne wa familia ya mgonjwa huyo anayetambuliwa kama Thomas Eric Duncan kutotoka nyumbani kwa siku 21 ili hali yao ya afya iweze kufuatiliwa kwa karibu.

Duncan aligunduliwa kuwa na kirusi cha Ebola Jumapili. Ametengwa na wagonjwa wengine katika hospitali ya Dallas huko Texas, ambako hali yake inaelezewa kuwa thabiti.

Huko London, waziri wa mambo ya nje Philip Hammond ametoa mwito wa hatua madhubuti ya kupambana na mlipuko wa Ebola ambao umeuwa zaidi ya watu 3,300 Afrika Magharibi.

Katika kongamano la kujadilia kirusi cha Ebola, waziri huyo alisema hatua kama hiyo itaokoa maisha ya maelfu ya watu na kuzuia mlipuko huo kusambaa zaidi.

Nalo shirika la afya duniani WHO, linasema zaidi ya watu 7,100 wameambukizwa kirusi cha Ebola na karibu wote wanatoka Sierra Leone, Guinea na Liberia.

XS
SM
MD
LG