Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 16:33

Marekani yamtaja Mtanzania kinara wa usafirishaji dawa za kulevya


Mifuko yenye dawa za kulevya aina ya heroin.
Mifuko yenye dawa za kulevya aina ya heroin.

Wizara ya fedha nchini Marekani imemtaja raia mmoja wa Tanzania, Ali Khatib Haji Hassan na mtandao wake kama “kinara wa usafirishaji wa dawa za kulevya” kwa kushiriki katika usafirishaji wa kimataifa wa dawa za kulevya.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Balozi Augustine Mahiga na kwanza kutaka kujua iwapo serikali ya Tanzania inafahamu lolote kuhusiana na harakati za raia huyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kwa hatua hiyo marekani ilimuwekea vikwazo Hassan na jamaa wanaohusika naye kwenye harakati hizo na kupoteza sifa ya kupata Viza ya kuingia Marekani.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani mjini Washington hapo Jumatano ilisema Hassan alikuwa akihusika katika usafirishaji wa shehena kubwa za dawa za kulevya kwenda mataifa ya Afrika, ulaya, Asia na Marekani.

Polisi wa kupambana na dawa za kulevya akifungua mzigo unaosadikiwa wa cocain
Polisi wa kupambana na dawa za kulevya akifungua mzigo unaosadikiwa wa cocain

Hassan alikamatwa na serikali ya Tanzania mwaka 2014 kwa kujaribu kuingiza kiasi cha kilogram 210 za dawa aina ya heroin mwaka 2012.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, bibi Virginia Blaser alisema katika taarifa yake kuwa Marekani imefurahi “kushirikiana kwa karibu na Tanzania katika kudhibiti vitisho vinavyotokana na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kama Hassan na mitandao ya kihalifu inayowasaidia”.

XS
SM
MD
LG