Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 22:56

Marekani imemuachia huru mfungwa wa Guantanamo raia wa Pakistan


Saif Ullah Paracha (katika picha isiyokuwa na tarehe) raia wa Pakistan ameachiwa huru kutoka gereza la Guantanamo Bay

Tangazo fupi la wizara ya mambo ya nje ya Pakistan siku ya Jumamosi lilithibitisha kurejeshwa kwa Saif Ullah Paracha, mwenye umri wa miaka 74, nchini mwake. "Tunafurahi kwamba raia wa Pakistan aliyekuwa kizuizini nje ya nchi hatimaye ameungana tena na familia yake," taarifa ilisema

Marekani imemuachia huru na kuhamishiwa Pakistan mmoja wa wafungwa wa nsiku nyingi sana waliobaki katika kituo cha siri cha Guantanamo Bay kinachoendeshwa na Marekani huko Cuba.

Tangazo fupi la wizara ya mambo ya nje ya Pakistan siku ya Jumamosi lilithibitisha kurejeshwa kwa Saif Ullah Paracha, mwenye umri wa miaka 74, nchini mwake. "Tunafurahi kwamba raia wa Pakistan aliyekuwa kizuizini nje ya nchi hatimaye ameungana tena na familia yake," taarifa ilisema.

Raia huyo wa Pakistan ni miongoni mwa takriban wanaume 40 waliokamatwa ambao kwa sasa wanazuiliwa katika gereza hilo la siri la Marekani. Inasemekana alikuwa miongoni mwa wafungwa wagonjwa sana huko.

Gereza lenye utata la Guantanamo wakati mmoja lilihifadhi mamia ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo waliokamatwa na vikosi vya Marekani nchini Afghanistan wakati wa "vita vya ugaidi" vya Washington dhidi ya mtandao wa kigaidi wa kigeni wa al-Qaeda. Vita hivyo vilianzishwa siku chache baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001 dhidi ya Marekani, ambapo maafisa walisema yalipangwa na viongozi wa al-Qaeda kutoka maeneo yao ya Afghanistan.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG