Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 08:29

Marekani na Australia zakubaliana kushiriki kijeshi


Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa Australia, Julia Gillard (R) wakiwa kwenye jengo la bunge la Australia huko Canberra. November 16, 2011

Marekani na Australia watiliana saini mkataba unaoruhusu majeshi ya Marekani katika ardhi ya Australia

Viongozi wa Marekani na Australia wametangaza mkataba wa kuweka majeshi ya Marekani katika ardhi ya Australia.

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa Australia, Julia Gillard, walizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkataba huo kufuatia mazungumzo yao ya Jumatano huko Canberra.

Gillard alisema mkataba utaruhusu kupelekwa kati ya wanajeshi 200 hadi 250 wa jeshi la Marines la Marekani katika kambi huko kaskazini mwa Australia na kubaki kwa zamu ya kipindi cha miezi sita. Aliongeza kuwa mkataba pia unaruhusu ndege za kijeshi za Marekani kutumia kambi za Australia.

Obama alisema mkataba utairuhusu Marekani kujibu vyema zaidi aina mbali mbali ya mahitaji ya kibinadamu na majanga pamoja na changamoto za usalama.
Obama alisema mkataba pia utasaidia kuendeleza mfumo wa usalama wa kanda ya Asia-Pacific. Alisema pia utarahisisha wanajeshi wa Marekani kufanya mafunzo na mazoezi pamoja na wanajeshi kutoka nchi nyingine katika kanda hiyo, na kupatia mataifa madogo vifaa kuweza kukabiliana na mizozo kwa haraka.

Rais Obama alisema anatumia ziara yake ya Australia, kueleza bayana kwamba Marekani inaongeza ushirikiano wake na kanda nzima ya Pacific, akisema “tuko hapa kubaki”

China ilijibu haraka tangazo la Canberra, ikidokeza kwamba kuweka majeshi ya Marekani huko Australia huwenda isiwe jambo la busara na inabidi lizungumziwe miongoni mwa jumuiya ya kimataifa.

Wafanyakazi wa Obama walisisitiza hakukuwa na jambo lisilo sahihi kuhusu mpango huo, lakini Rais wa Marekani hakujibu moja kwa moja wakati alipoulizwa kama mpango huo ulikuwa majibu ya China kuongeza nguvu za kijeshi.

XS
SM
MD
LG