Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 23, 2025 Local time: 18:06

Mapigano Sudan yaingia wiki ya pili kati ya vikosi vya majenerali hasimu


Kamanda wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel-Fattah Burhan akizungumza katika eneo lisilowekwa bayana huko Sudan. April 21, 2023.
Kamanda wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel-Fattah Burhan akizungumza katika eneo lisilowekwa bayana huko Sudan. April 21, 2023.

Milio mizito ya risasi, milipuko mikubwa, na ndege za kivita zilinguruma katika maeneo mengi ya mji mkuu Jumamosi asubuhi kulingana na mashuhuda.

Mapigano katika mji mkuu wa Sudan yaliingia wiki ya pili Jumamosi wakati milio ya risasi ikivunja makubaliano ya muda ya sitisho la mapigano, mapambano ya hivi karibuni kati ya vikosi vya majenerali hasimu tayari yamesababisha vifo vya mamia ya watu na maelfu kujeruhiwa.

Usiku wa kuamkia Jumamosi milipuko mizito ambayo awali iliutikisa mji katika siku za hivi karibuni ilikuwa imepungua lakini Jumamosi asubuhi mapigano yalianza tena. Milio mizito ya risasi, milipuko mikubwa, na ndege za kivita zilinguruma katika maeneo mengi ya mji mkuu Jumamosi asubuhi kulingana na mashuhuda.

Ghasia ziliibuka Aprili 15 kati ya vikosi vinavyomtii mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake aliyegeuka kuwa hasimu wake Mohamed Hamdan Daglo ambaye anaongoza vikosi vyenye nguvu vya Rapid Support Forces (RSF).

XS
SM
MD
LG