Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:11

Mapigano mepya yazusha vifo zaidi Sudan Kusini


Wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini katika mji wa Koch Sept 25, 2015.
Wanajeshi wa serikali ya Sudan Kusini katika mji wa Koch Sept 25, 2015.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini Lul Ruai Koang alisema Jumapili kuwa mapigano makali yamezuka karibu na mji wa Malakal mwishoni mwa wiki na kusababisha vifo vya darzeni ya watu baada ya waasi kusema watajaribu kuchukua udhibiti wa mji huo.

Jeshi lilieleza kwamba waasi walishambulia vituo vya serikali Ijumaa usiku lakini jeshi liliweza kulinda maeneo linaloshikilia. Taarifa ya jeshi iliendelea kueleza kwamba “wanajeshi wetu walifanikiwa kuwarudisha nyuma waasi na kusababisha vifo vingi”.

Zaidi ya waasi 56 waliuwawa. Idadi kamili ya vifo haikuweza kuthibitishwa lakini mpiga picha wa shirika la habari la Reuters ambaye alisafiri na jeshi kuelekea Lalo kambi iliyo jirani na Malakal aliona miili 15 karibu na jengo moja lililochomwa ndani ya kituo hicho na miili iliyokatwa katwa katika maeneo mengine.

Ghasia za kisiasa huko Sudan Kusini
Ghasia za kisiasa huko Sudan Kusini

Wanajeshi walisema walikuwa wakitarajia shambulizi jingine. Ijumaa, waasi walisema waliuteka mji wa Lalo na eneo jirani la Wajwok na pia wanapanga kuuteka mji wa Malakal.

Ripoti hiyo imetolewa wakati idara ya Umoja wa Mataifa inayowashughulikia wakimbizi- UNHCR inaeleza kwamba idadi ya wakimbzii wa Sudan Kusini wanaoingia Uganda inaongezeka na imefikia milioni moja.

XS
SM
MD
LG