Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 08:22

Mali:Cisse apongeza Boubacar Keita


Ibrahim Boubacar keita
Ibrahim Boubacar keita
Mgombea urais nchini Mali Soumalia Cisse amekubali kushindwa na mpinzani wake Ibrahim Boubacar Keita katika duru ya pili ya uchaguzi uliofanyika Jumapili. Akizungumza Jumatatu jioni Cisse alisema bw.Keita alishinda uchaguzi huo kwa njia halali na kumtakia kila la kheri.

Msemaji wa bw.Keita, Mamadou Camara alisema matokeo yanaonyesha kuwa alipata kati ya asili mia 70 na 80 ya kura.Camara alisema bw. Cisse alimtembelea Keita nyumbani kwake Jumatatu jioni na kumpongeza kufuatia ushindi huo.

Akizungumza na idhaa ya Kifaransa ya Sauti ya Amerika Jumanne msemaji huyo alisema kuwa ushindi wa bw. Keita ulikuwa mkubwa na kwamba sasa ataelekeza nguvu zake zote katika kuleta maridhiano ya kitaifa nchini Mali.
XS
SM
MD
LG