Baadhi ya viongozi wa kikanda barani Afrika wametia saini makubaliano yaliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa Jumapili, kwa lengo la kumaliza mtafaruku wa miongo miwili katika eneo la mashariki la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Makubaliano hayo yametiwa saini katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon alihudhuria sherehe hizo pia na kusema makubaliano hayo ni mwanzo wa mchakato wa kufikia maelewano ya kudumu.
Inategemewa makubaliano hayo pia yatakuwa chanzo cha kuunda kikosi cha kikanda kupambana na waasi katika eneo hilo lenye utajiri wa madini la DRC mashariki.
Viongozi hao wa Afrika walitegemewa kutia saini makubaliano hayo mwezi jana lakini yakaahirishwa baada ya kuibuka wasiwasi juu ya nani atakayeoongoza kikosi hicho cha kikanda.
Viongozi wa ukanda wa maziwa makuu watakutana tena Kampala, Uganda Machi 15 kuendelea na majadiliano ya kusuluhisha mzozo baina ya serikali ya Kinshasa na kundi la waasi wa M23.