Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 14:08

Majeshi ya usalama Nigeria yamkamata ofisa wa zamani wa jeshi


Chris Olukolade(L), mkurugenzi wa idara ya ulinzi Nigeria na Mike Omeri, mratibu katika idara hiyo.
Chris Olukolade(L), mkurugenzi wa idara ya ulinzi Nigeria na Mike Omeri, mratibu katika idara hiyo.

Majeshi ya usalama nchini Nigeria yamemkamata ofisa wa zamani wa jeshi wa upelelezi ambaye anashutumiwa kwa kupanga ulipuaji bomu katika mji mkuu ambalo liliuwa darzeni ya watu.
Katika saa za mapema hapo April 14, kituo cha basi cha Nyanya kilichopo nje ya Abuja kilijaa wasafiri wakielekea kazini kati kati ya mji wakati mabomu mawili yalipoteguliwa. Kiasi cha watu 71 waliuwawa na mamia zaidi walijeruhiwa.

Milipuko ilikuwa tukio la kwanza kutokea katika mji mkuu katika kipindi cha miaka miwili na kusababisha vifo vingi katika historia ya mji.

Majeshi ya usalama ya Nigeria yaliwakamata washukiwa watano mwezi mei wakisema wawili wengine waongozaji wa mpango huo hawajulikani walipo.

Msemaji wa idara ya usalama wa taifa, Marilyn Ogar anasema mmoja wa washukiwa hao, Aminu Sadiq Ogwuche, alirudi Nigeria siku ya Jumanne. “Majeshi ya usalama yalimpokea Aminu Sadiq Ogwuche, ambaye amerejeshwa na serikali ya Sudan na tangu wakati huo yuko chini ya ulinzi. Uchunguzi unaendelea kufanyika na ninafikiri hivi karibuni atashtakiwa mahakamani”.

Ogwuche alizaliwa Uingereza, ni mtoto wa kiume wa kanali mstaafu wa jeshi la Nigeria. Awali ameshakamatwa kwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi.

Maafisa wanasema kukamatwa kwake ni ushindi mkubwa kwa majeshi ya usalama ya Nigeria ambayo yamekuwa yakikosolewa vikali kwa kushindwa kuwaokoa Zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara huko kaskazini, siku hiyo hiyo ambayo bomu lili-lipuka Nyanya.

Kundi la Boko Haram
Kundi la Boko Haram

Kundi la wanamgambo la Boko haram lilidai kuhusika na shambulizi la bomu na utekaji nyara wa wasichana. Kundi hilo linasema linataka kusimika sheria kali za ki-Islam Nigeria na linalaumiwa kwa maelfu ya vifo, mwaka huu pekee.

Tangu Nyanya kulipuliwa, mabomu menginemawili huko Abuja yamesababisha darzeni ya vifo na kuongeza khofu kwamba Boko Haram linapanuka mbali ya eneo la kaskazini-mashariki ambako majimbo matatu yamekuwa chini ya utawala wa dharura kwa zaidi ya mwaka mmoja.

XS
SM
MD
LG