Jaji Lewis Kaplan akiwa kwenye mahakama ya Manhattan, New York, amepinga ombi la Trump kwamba alikuwa analindwa dhidi ya mashitaka kutokana na cheo chake cha urais. Trump alidai kwamba Carroll alisubiri kwa miongo kadhaa kabla ya kuwasilisha malalamishi yake na kwa hivyo hakuwa na budi ila kujitetea.
Mawakili wa Trump wala wa Carroll hawajasema lolote kutokana na hatua hiyo. Carroll alifunguka mara ya kwanza hapo Juni 2019, pale aliposhtumu Trump kwamba alimshambulia kwenye chumba cha kujaribia mavazi kwenye duka la Bergdorf Goodman, kwenye kitongoji cha Manhattan, wakati Trump akikanusha kumfahamu na kusema kwamba Carroll hakuwa aina ya wanawake awapendao.
Carroll anaomba kulipwa ridhaa ya takriban dola milioni 10, na kesi yenyewe imepangwa kusikilizwa Januari 15 mwaka ujao.
Forum