Mahakama ya juu ya Finland imezuia kusafirishwa kwa raia wa Russia wa neo-Nazi kwenda Ukraine, ambako anatakiwa kwa mashtaka ya kigaidi. Jan Petrovsky anatuhumiwa kushiriki katika kundi la kigaidi nchini Ukraine.
Mahakama ya Finland ilizuia kupelekwa kwake kwa sababu iliamini kuwa atakuwa chini ya hali ya kudhalilisha katika gereza la Ukraine. Petrovsky, mamluki wa zamani wa Wagner Group aliachiliwa kutoka gereza la Finland, lakini aliwekwa chini ya ulinzi na walinzi wa mpaka wa Finland.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema katika hotuba yake ya kila siku hapo Ijumaa kwamba kulikuwa na shambulio la kombora katika mikoa ya Kharkiv na Dnipropetrovsk siku ya Ijumaa asubuhi, lakini sehemu kubwa ya makombora ya Russia yalifanikiwa kuzuiwa. Alisema mtu mmoja aliuawa.
Forum