Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 00:25

Mahakama moja ya CAR yatoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo


Magari ya rais wa zamani wa Afrika Kati, aliyekuwa uhamishoni Francois Bozize yakiwa yameegeshwa ikulu huko Bangui, Machi 25 2013. Picha na REUTERS/Ange Aboa.
Magari ya rais wa zamani wa Afrika Kati, aliyekuwa uhamishoni Francois Bozize yakiwa yameegeshwa ikulu huko Bangui, Machi 25 2013. Picha na REUTERS/Ange Aboa.

Mahakama moja inayoungwa mkono kimataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati siku ya Jumanne ilitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, aliye uhamishoni, François Bozize, kwa ukiukaji wa haki za binadamu kuanzia mwaka 2009 hadi 2013, msemaji wao alisema.

Msemaji wa mahakama Gervais Bodagy Laoulé alisema hati hiyo ni ya uhalifu uliofanywa chini ya uongozi wa Bozize katika gereza la kiraia na katika kituo cha mafunzo ya kijeshi katika mji wa Bossembelem ambapo watu wengi waliteswa na kuuawa.

Hati hiyo inashughulikia uhalifu kutoka mwaka 2009 hadi 2013 na walinzi wa rais na vikosi vingine vya usalama, Laoule alisema.

Bozizé kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Guinea Bissau, ambapo Rais wa nchi hiyo Umaro Sissoco Embaló aliliambia Shirika la Habari la Associated Press kwamba hajapokea ombi lolote kutoka Bangui kuhusu hati ya kukamatwa kwake, na kwamba sheria za nchi hiyo haziruhusu kurejeshwa mtu ili aweze kushitakiwa.

Forum

XS
SM
MD
LG