Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 02:29
VOA Direct Packages

Mahakama kuu ya Marekani yasikiliza kesi ya kulinda makampuni ya Internet dhidi ya mashitaka


Nembo za baadhi ya makampuni yanayolindwa na sheria hiyo.

Mahakama ya juu ya Marekani Jumanne imesikiliza kwa mara ya kwanza kesi huhusu sheria ya serikali kuu, iliyosaidia kutengeneza internet, kwa kulinga makampuni makubwa ya teknolojia ya mawasiliano kama vile Google, Twitter na Facebook miongoni mwa mengine

Sheria hyo imekuwa ikitumika kulind makampuni hayo dhidi ya kushitakiwa kutokana na taarifa zinazorushwa kupitia majukwaa yake. Majaji wa mahakama hiyo wamesikiliza hoja ya iwapo familia ya kimarekani ya mwanafunzi wa chuo aliyeuwawa kwenye shambulizi la kigaidi mjini Paris, inaweza kushitaki Google kwa kusaidia magaidi kueneza ujumbe wao na kuvutia vijana wapya kujiunga nao.

Hiyo ndiyo kesi ya kwanza inayomulika sheria ya maadili ya mawasiliano nambari 230, iliyopitishwa 1996, kwa nia ya kulinda makampuni dhidi ya mashitaka kutokana na taarifa zinazowekwa kwenye mitandao yao. Mahakama za chini zimetetea sheria hiyo zikisema kwamba inalinda sekta ya internet, huku makampuni ya mawasiliano pamoja na washirika wao wakisema kwamba imechochea ukuaji wa Internet pamoja na kudhibiti ujumbe hatari kuwekwa kwenye mitandao.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG