Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 15:01

Maandamano yaendelea Sudan kupinga utawala wa kijeshi


Waandamanaji mitaani wakipinga utawala wa kijeshi kutwaa madaraka Khartoum Sudan. (Picha na AFP)

Waandamanaji walionyesha ukaidi  katika mitaa ya Sudan mapema Jumanne wakiandamana kupinga mapinduzi ya kijeshi,

Waandamanaji walionyesha ukaidi katika mitaa ya Sudan mapema Jumanne wakiandamana kupinga mapinduzi ya kijeshi, huku jumuiya ya kimataifa ikiendelea kulaani vikosi vya usalama vya nchi hiyo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likitarajiwa kukutana baadaye.

Barabara zilifungwa, maduka yalifungwa, simu zilizimwa na vipaza sauti vya msikitini vilitoa wito wa kufanyika kwa mgomo mkubwa nchini humo siku moja baada ya jeshi kuchukua mamlaka katika mapinduzi yaliyosababisha machafuko ambapo takriban watu saba waliuawa.

Kurudi nyuma sio jambo linalokubalika, ni maneno waliokua wanatamka waandamanaji waliokaidi amri ya wanajeshi walokua wanafyatua risasi mapema Jumanne kujaribu kuwatawanya na inaripotiwa kuwaua watu watatu.

Moshi mwingi ulitanda Khartoum kutokana na matairi yaliyochomwa moto na waandamanaji. Maisha yalisimama katika mji mkuu Khartoum na katika mji wake pacha wa Omdurman ng'ambo ya Mto Nile, huku barabara zikiwa zimefungwa na wanajeshi au vizuizi vya waandamanaji.

Usiku ulionekana kupita kwa utulivu ukilinganisha hali baada ya machafuko ya Jumatatu, wakati waandamanaji walipoingia barabarani baada ya wanajeshi kumkamata Waziri Mkuu Abdalla Hamdok na raia wengine katika baraza la mawaziri. Afisa wa wizara ya afya ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu saba wameuawa katika makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

Sudan ilikuwa katika hali mbaya tangu kushindwa kwa njama ya mapinduzi mwezi mmoja tu kabla.

Makundi ya kijeshi na ya kiraia yamekuwa yakishirikiana kwenye madaraka kufuatia kupinduliwa kwa kiongozi wa kiimla Omar al-Bashir miaka miwili iliyopita.

Jeshi lilikusudiwa kukabidhi madaraka kwa mtu atakayechaguliwa katika miezi ijayo.

Siku ya Jumatatu, vugu vugu la FFC lilitoa wito kwa nchi nzima kutotii sheria na kugoma.

Muandamanaji anayeunga mkono utawala wa kiraia alisema hawataondoka barabarani hadi serikali ya kiraia irudi,

Siku ya Jumatatu Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitoa taarifa ya pamoja iliyotiwa saini na Uingereza na Norway kulaani mapinduzi hayo.

Akizungumza Jumatatu jioni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alielezea wasiwasi wake kuhusu ripoti kwamba vyombo vya usalama vilitumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG