Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 08:22
VOA Direct Packages

Maandamano Morocco kuhusiana na kesi ya ubakaji ya msichana wa miaka 11


Watu waandamana Casablanca, Morocco kwenye picha ya maktaba.
Watu waandamana Casablanca, Morocco kwenye picha ya maktaba.

Waandamanaji nchini Morocco Jumatano wamelalamikia uamuzi wa mahakama kwa kesi ya ubakaji iliyowahusisha  wanaume watatu dhidi ya msichana mwenye umri wa miaka 11 na ambayo imetia doa taifa hilo.

Kwa mijibu wa shirika la habari la AFP, rufaa iliyokatwa na msichana huyo dhidi ya uamuzi wa Machi 20, wa mahakama ya rufaa iliyotoa hukumu ya kifungo cha miaka 2 jela kwa mshukiwa mmoja, na miezi 18 jela kwa wenzake wawili, huenda ikaakhirishwa kutokana na ombi la wakili wa msichana huyo.

Msichana huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 12 kutoka kijiji kilichoko karibu na mji wa Rabat inasemekana alibakwa ndani ya kipindi cha miezi kadhaa, kulingana na taarifa ya mwezi uliopita, kutoka shirika la wanawake wa Morocco la Jossour.

Sheria za Morocco zinaruhusu kifungo cha hadi miaka 20 kwa hatia kama inayowakabili wanaume hao, ambao pia watalipa jumla ya dirham 50,000 ambazo ni sawa na dola 4,880 za kimarekani kama fidia. Mmoja wa washukiwa anasemekana kumbebesha mimba msichana huyo, kulingana na mtandao wa habari wa Media24.

XS
SM
MD
LG