Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:47

Maandamano makubwa yafanyika Ufaransa kupinga ugaidi


Rais wa ufaransa Francois Hollande akiwa amezungukwa na viongozi wa dunia kwenye maandamano katika mitaa ya Paris.
Rais wa ufaransa Francois Hollande akiwa amezungukwa na viongozi wa dunia kwenye maandamano katika mitaa ya Paris.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameongoza maelfu ya watu kwenye mitaa ya Paris Jumapili , katika maandamano makubwa ya kuonyesha umoja na waathiriwa wa shambulizi la kigaidi la Januari 7 lililouwa watu 17.

Viongozi wa dunia waliungana na Bwana Hollande katika mji mkuu wakati kundi la watu likihamasisha umoja kwenye maandamano kote katika mitaa.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron , kansela wa Ujerumani Angela Markel, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Rais wa Palestina Mahmoud Abbas pamoja na mfame na mama mfalme wa Jordan pia walishiriki katika maandamano hayo.

Maafisa wa Ufaransa wameita mauaji ya Januari 7 katika ofisi za Paris kwenye gazeti la Charlie Hebdo na mfululizo wa mashambulizi mengine ya mauaji ni ya kigaidi.

Wakati huo huo mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder alitangaza kutoka Paris Jumapili kwamba rais Barack Obama atakaribisha viongozi wa dunia mjini Washington, February 18 katika mkutano wa kupinga ghasia zenye msimamo mkali.

XS
SM
MD
LG