Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 13:09

Maafisa wa UN wamependekeza kikosi maalum kwa ajili ya kurejesha usalama nchini Haiti


Waandamanaji wakiwa wamewasha moto katikati ya barabara kwenye mji mkuu wa Haiti
Waandamanaji wakiwa wamewasha moto katikati ya barabara kwenye mji mkuu wa Haiti

Maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wameiomba jumuia ya kimataifa kutuma kikosi maalum nchini Haiti kama hatua ya kurejesha hali ya kawaida kwenye taifa hilo la Caribbean.

Ripoti zinasema kwamba ukosefu wa usalama kwenye taifa hilo umefika kwenye viwango vya kutisha. Wakati akiwasilisha hoja yake mbele ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, naibu katibu mkuu Amina J. Mohhamed amesema kwamba ingawa kulikuwa na matumaini mwaka mmoja uliopita wa mageuzi ya kisiasa, uthabiti na maendeleo ifikapo mwisho wa mwaka 2022, Haiti imeendelea kugubikwa na kiwango kikubwa cha mzozo usiotarajiwa na kutia wasi wasi mkubwa sana.

Akiripoti kwa baraza hilo kwa njia ya video kutoka Haiti, mkuu wa ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa nchini humo Helen la Lime, ametoa takwimu za kutisha kwa kusema kwamba katika mwezi Novemba pekee, mauaji 280 yameripotiwa wakati mengine 1,200 yakiripotiwa mwaka huu, ikiwa idadi ikiongezeka mara mbili ikilinganishwa na mwaka 2021.

XS
SM
MD
LG