Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 07, 2024 Local time: 00:03

Maafisa Marekani wataja tukio la kwanza duniani la mtu kuambukizwa mafua ya ndege kutoka kwa mnyama

Ng'ombe wanaonekana kwenye kiwanda cha maziwa huko California. Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani ilisema Jumanne, Aprili kwamba sampuli za maziwa zilipatikana na mabaki ya virusi vya mafua ya ndege ambayo yameambukiza ng'ombe wa maziwa.

Mfanyakazi mmoja wa shamba la Michigan amegunduliwa ana ugonjwa wa mafua ya ndege ikiwa ni kisa cha pili cha binadamu kuhusishwa na mlipuko katika  eneo lenye  ng'ombe wa maziwa Marekani.

Maafisa wa afya wanasema mtu huyo alipata dalili za ugonjwa wa macho kidogo na amepona. Maafisa wanasema mfanyakazi huyo alikuwa karibu na ng'ombe kwenye shamba lililokuwa na mifugo iliyoambukizwa.

Maafisa wanasema hatari kwa umma bado ni ndogo, lakini wafanyakazi wa shamba walio karibu na wanyama walioambukizwa wako katika hatari kubwa zaidi.

Mfanyakazi mmoja wa shamba la Texas aligunduliwa mwishoni mwa Machi katika hali kama hiyo. Maafisa walitaja tukio hilo la kwanza kujulikana duniani kote la mtu kuambukizwa aina hii ya mafua ya ndege kutoka kwa mnyama.

Forum

XS
SM
MD
LG