Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 14:50

Kamanda wa kundi la uasi la LRA akamatwa


Caesar Achellam, kamanda wa cheo cha juu wa kundi la LRA
Caesar Achellam, kamanda wa cheo cha juu wa kundi la LRA

Mapambano makali kati ya majeshi ya serikali na uasi yamepelekea kukamatwa kwa Caesar

Jeshi la Uganda linasema limemkamata kamanda mmoja wa kundi la waasi wa Uganda - Lord’s Resistance Army wakati wa operesheni za kijeshi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Caesar Achellam alitenaswa Jumamosi wakati wa mapigano makali baina ya waasi na vikosi vya Uganda.

Kukamatwa kwa Caesar Achellam huko Jamhuri ya Afrika ya kati, ni ushindi mkubwa kwa vikosi vya pamoja kutoka matiafa mbalimbali, vinaoshirikiana kupambana na kundi la LRA kote huko Afrika ya kati. Kituo cha operesheni huko Jamhuri ya Afrika ya kati kwa ushirikiano na jeshi la Uganda na vikosi maalum vya kimarekani, wamebandika picha ya Achellam ukutani, karibu na picha za viongozi wengine wa LRA, ikiwa ni pamoja na kiongozi wa kundi hilo la waasi, Joseph Kony.

Shirika la habari la Reuters, lilimnukuu msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulaigye, akimuelezea Achellam kuwa ni mojawapo wa viongozi wakuu wa LRA. Jeshi hilo linasema alikamatwa huko Jamhuri ya Afrika ya kati, mojawapo ya nchi ambazo kundi la LRA linajulikana kuendesha operesheni zake.

Kundi hilo wakati mmoja lilikuwa na maelfu ya wafuasi , lakini maafisa wa kijeshi wa Marekani na Uganda, wanaamini kuna wapiganaji mia kadhaa tu waliobakia.

Kundi hilo lina umaarufu wa kuteka nyara watoto na kuwatumia kama wanajeshi, wachukuzi na watumishi wa ngono. Maelfu wametekwa nyara tangu kundi hilo kuanza uasi wao huko Uganda zaidi ya miaka 25 iliyopita.

XS
SM
MD
LG