Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 16:26

Liberia yatangaza hali ya dharura kutokana na Ebola


Wahudumu wa afya ndani ya jengo linalowahudumia wagonjwa wa Ebola.
Wahudumu wa afya ndani ya jengo linalowahudumia wagonjwa wa Ebola.

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza hali ya dharura wakati mlipuko wa Ebola ukiendelea kusababisha vifo kwa maelfu ya watu nchini mwake na mataifa mengine ya Afrika magharibi.

Katika hotuba yake kwa taifa Jumatano jioni Bibi Sirleaf alisema Liberia lazima ichukue hatua mbadala za ziada kulinda maisha ya watu na kulinusuru taifa.

​Hatua hizo zitajumuisha kutumia majeshi ya usalama kuweka karantini kwa maeneo yaliyoathirika na kudhibiti mienendo ya watu.

Shirika la habari la Uingereza-Reuters linaripoti kwamba polisi na wanajeshi katika nchi jirani ya Sierra leone wamezuia maeneo kadhaa ya vijijini katika juhudi za kuzuia ugonjwa wa Ebola kutosambaa zaidi katika nchi hiyo.

Shirika la afya Duniani-WHO linasema ugonjwa wa Ebola umeuwa zaidi ya watu 930 huko Afrika magharibi hasa katika nchi ya Liberia, Sierra leone na Guinea. Idadi jumla ya kesi ipo katika kiwango cha zaidi ya 1,700.

Wakati huo huo WHO inasema kwamba wiki ijayo itakutana pamoja na jopo la sheria kuzungumzia utumiaji wa vifaa vya matibabu kwa ugonjwa wa Ebola.

Shirika hilo katika Umoja wa Mataifa linasema utumiaji wa dawa kwa raia wawili wa Marekani umezua maswali kuhusu kama dawa isiyofanyiwa majaribio itumike katika kutibu mlipuko wa Ebola na kama inatumika nani anatakiwa kupatiwa dawa hiyo.

XS
SM
MD
LG